Mhandisi mkazi John Mageni kutoka katika mradi wa ujenzi wa umeme wa Mwalimu Nyerere JNHPP katika hifadhi ya Mwalimu Nyerere wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani ameieleza Ayo TV kua upembuzi akinifu uliyotumika ni wa mwaka 2017 ambao ulibadilishwa vitu vingi kutoka upembuzi akinifu wa mwaka 1980 ambao ulipangwa ujenzi huo uanze. Hayo ameongea baada ya kusikika kwa taarifa kua mradi huo unatumia upembuzi akinifu wa mwaka 1980 badala ya mpya ambao ulipaswa kutengenezwa..